2 Thessalonians 3

1Na sasa, ndugu, tuombeeni, kwamba neno la Bwana liweze kuenea na kutukuzwa, kama ilivyo pia kwenu. 2Ombeni kwamba tuweze kuokolewa kutoka katika uovu na watu waasi, kwa kuwa si wote wana imani. 3Lakini Bwana ni mwaminifu, ambaye atawaimarisha ninyi na kuwalinda kutoka kwa yule mwovu.

4Tunaujasiri katika Bwana kwa ajili yenu, kwamba mnatenda na mtaendelea kutenda mambo ambayo tunawaagiza. 5Bwana aweze kuongoza mioyo yenu katika upendo na katika uvumilivu wa Kristo.

6Sasa tunawaagiza, ndugu, katika jina la Bwana Yesu Kristo, kwamba mwepuke kila ndugu ambaye anaishi maisha ya uvivu na siyo kwa kutokana na desturi ambazo mlipokea kutoka kwetu. 7Kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua ni sawa kwenu kutuiga sisi. Hatukuishi miongoni mwenu kama wale ambao hawakuwa na nidhamu. 8Na hatukula chakula cha mtu yeyote bila kukilipia. Badala yake, tulifanya kazi usiku na mchana kwa kazi ngumu na kwa shida, ili tusiweze kuwa mzigo kwa yeyote katika ninyi. 9Tulifanya hivi si kwa sababu hatuna mamlaka. Badala yake, tulifanya hivi ili tuwe mfano kwenu, ili kwamba mweze kutuiga sisi.

10Wakati tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaagiza, “Ikiwa mmoja wenu hataki kufanya kazi, na asile.” 11Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi wanaenenda kwa uvivu miongoni mwenu. Hawafanyi kazi lakini badala yake ni watu wasio na utaratibu. 12Sasa hao nao tunaagiza na kuwaasa katika Bwana Yesu Kristo, kwamba lazima wafanye kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.

13Lakini ninyi, ndugu, msizimie roho katika kufanya yaliyo sahihi. 14Ikiwa mtu yeyote hataki kutii neno letu katika waraka huu, mwe makini naye na msiwe na ushirika pamoja naye, ili kwamba aweze kuaibika. 15Msimchukulie kama adui, lakini mwonyeni kama ndugu.

16Bwana wa amani mwenyewe awape amani wakati wowote katika njia zote. Bwana awe nanyi nyote. 17Hii ni salam yangu, Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe, ambayo ni alama katika kila waraka. Hivi ndivyo niandikavyo. 18Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iweze kuwa nanyi nyote.

Copyright information for SwaULB